Ni Jukwa la kukutanika. Kubadilishana mawazo na kukuzana.
WeCie ni mtandao ulioanzishwa kwa madhumuni ya kuzidisha kuangazia kazi ambazo wanawake wa tabaka tofauti walio na tajriba mbali mbali wanazofanya kuhusiana na kukomesha dhuluma za kijinsia wakati wa dharura au wakati kunapokuwa na vita katika nchi zao au kwingineko. Jukwaa hili linatoa nafasi ya watu binafsi walio na tajriba mbalimbali kukutana na wanawake wa tabaka tofauti duniani kote, ili kubadilishana mawazo na kushiriki mambo ambayo wamepitia maishani, kubadilishana njia za kusuluhisha matatizo, kubadilishana raslimali na kushirikiana ili kujaza nafasi zinazojitokeza ili kujiendeleza. Kama ungependa kujua mengi kuhusu wanachama wetu basi tafadhali bonyeza na uingie kwenye ukurasa wetu ili usome wasifu na ujuzi wao katika mtandao wa kila mmoja wao uliowekwa wazi kwa kila mtu, pia nenda ubonyeze kwa ukurasa ulio na nembo “OurView” ili usome, utazame au usikilize kutoka kwa wanachama wetu moja kwa moja.Kama wewe ni mwanamke wa tabaka tofauti na unafanya kazi katika nyanja ya kupinga dhuluma za kijinsia wakati wa dharura basi jukwaa hili liliundwa kihususa kwa ajili yako na tunatarajia kukutana na wewe katika mtandao huu wetu.
Jiunge nasi kwa kubonyeza hapa. Tunatazamia kukukaribisha kwa majukwaa yetu na kuonana na wewe katika matukio yetu ya hivi karibuni.