top of page

WANACHAMA NA JUKWAA LETU

WeCiE iliundwa kwa sababu ya uhitaji wa kuwa na jukwaa lililo salama na mahali ambapo watu wanaweza kukutanika kwenye mtandao ili kujadiliana na kubadilishana mawazo, kuuliza maswali na kubadilishana ujuzi tulionao, maazimio tuliyo nayo na masuluhisho yanayotumika kwa matatizo tuliyo nayo pamoja na wengine.

Mara nyingi hatutambuliki na hatusikiki, jukwaa hili linaongozwa na sauti za wanawake wa tabaka tofauti ambao ujuzi wao wa miaka mingi, tajriba yao, na suluhu zinazotumika zilihitaji juwaa la kubadilishana, kutambuliwa, na kwa njia ya pamoja kutambulisha na kudhihirisha wazi mchango wa wanawake wa tabaka tofauti na uongozi wao ili kuendeleza kazi ya kupinga dhuluma za kijinsia wakati wa dharura kwa pamoja na kwa ajili yetu sote.

Kama ulikuwa kwa nyanja hii kwa muda mrefu ama ndio mwanzo unaingia kwa uwanja huu – karibu ujiunge na wanawake wa tabaka tofauti wakati wa dharura. Hili ni jukwaa lako huru na salama kwa ajili ya kujieleza.  Tafadhali jisikie huru na usisite kujieleza hisia zako. Tuko na sheria moja tu: Uwe mnyenyekevu, mpole na mvumilivu.

SHERIA ZA JUKWAA

Jinsi ya kujiendesha kwenye jukwaa

WANACHAMA

Kama unafanya kazi katika Nyanja ya kukomesha dhuluma za kijinsia wakati wa dharura basi bonyeza hapa ili ujiunge nasi /bonyeza hapa ili ukutanike na wanachama wenzako.

Tazama na ufuate wanachama wengine kwenye mtandao, chapisha maoni yako na mengineyo.

UWE MNYENYEKEVU, MPOLE NA MVUMILIVU

Hili ni jukwaa lako huru na salama kwa ajili ya kujieleza. Tuko na sheria moja tu: Uwe mvumilivu, mnyenyekevu na mpole. Sote tunatoka malezi tofauti ya kijinsia, kimawazo, sehemu na tamaduni tofauti tofauti. Mtandao ulio na nguvu na wenye kushikamana ni ule ambao wanachama wake wanaweza kukubali na kutofautiana kimaoni na kimawazo bila kutengana. Acheni tuazimie jambo hilo.

forweb2islamic-women-friends-working-tog
forwebpregnant-women-in-class-PCWHT2J.jp

NI NINI KINACHOWEZA KUACHA UTOLEWE KWENYE MTANDAO HUU?

Ili mradi wewe unaheshimu maoni ya wengine, unachukua wakati wako kumsikiliza mwenzako kwa makini hata kama hukubaliani na maoni yake; na sote tunajitahidi sana kutoonyesha ubaguzi wa aina yoyote ile, basi utaendelea kukubalika katika jukwaa hili.  Tunatumaini kwamba hakuna hata mmoja wetu atakeyebidi kutolewa kwenye jukwaa hili.

bottom of page