top of page

KUTUHUSU

Hili ni Jukwa la kukutanika, kubadilishana mawazo na kukuzana.

Lengo kuu la mtandao huu ni ili kubuni uhusiano wa nguvu usio rasmi kati ya wanawake wa tabaka tofauti ulimwenguni kote wanaofanya kazi ya kukomesha duhuluma za kijinsia – mara nyingi katika sehemu zilizo na utata kwa sababu ya vita na hali za dharura. Kazi yetu inaweza kuwa ngumu na yenye upweke hasa kama wewe peke yako ndiye mwenye tajriba na zaidi ikiwa wewe uko peke yako na ni mwanamke uliye wa tabaka tofauti katika hilo eneo ambalo hutambuliki.

Mtandao huu ni ili kuangazia na kukusaidia katika hiyo hali ya upweke, kutotambuliwa na mengi zaidi.

Ni tumaini letu kwamba baada ya muda kupitia sisi sote katika mtandao huu wetu, tutaweza kuunda kongamano la kubadilishana ustadi wetu ili kudhihirisha na kutambulisha kazi yetu kupitia mitandao tofauti tofauti na majukwaa ya mtandaoni ya kila aina. Kama ungependa kujua mengi kuhusu wanachama wetu basi tafadhali bonyeza na uingie kwenye ukurasa wetu ili usome wasifu, tajirba na ujuzi wao katika mtandao wa kila mmoja wao uliowekwa wazi kwa kila mtu, pia nenda ubonyeze kwa ukurasa ulio na nembo “OurView” ili usome, utazame au usikilize kutoka kwa wanachama wetu moja kwa moja.

Kama wewe ni mwanamke wa tabaka tofauti na unafikiria kujiunga nasi tunatarajia kwamba hutasita. Basi tafadhali bonyeza hapa ili ujiunge nasi.

Tunatarajia kwa hamu kukukaribisha kwa jukwaa letu na kuonana na wewe katika matukio na shughuli zetu mbalimbali.

forwebwoman-using-computer-in-work-CATLD

JINSI YA KUWASILIANA/

UTAMBULISHO WAKO

Asante!

bottom of page